August 20, 2016WAKATI timu yake ikijiandaa kufungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, leo Jumamosi, Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, ametamba kuwa kikosi chake kimeiva na kipo fiti kwa ajili ya ligi.
Simba inatarajiwa kufungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa kuvaana na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Akizungumza  Omog alisema ana matumaini makubwa ya kupata ushindi kwenye mechi yao na Ndanda, hiyo ni kutokana na maandalizi aliyoyafanya.
“Ninaweza nikatamka kuwa, kikosi changu kimeiva hivi sasa, hiyo ni kutokana na maandalizi ya kutosha niliyoyafanya kuhakikisha tunauchukua ubingwa wa ligi kuu,” alisema Omog.
 

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Ndanda FC, Joseph Lazaro, naye alitamba kuwa usajili na maandalizi ya timu yake yanatosha kabisa.
 

“Simba hatuwaogopi, bali tunawaheshimu kutokana na ukongwe wao zaidi yetu, hivyo sisi tutaingia uwanjani kwa ajili ya ushindi, ninaamini usajili tulioufanya umekidhi vigezo,” alisema Lazaro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV