August 15, 2016


Beki wa kati wa Yanga, Andrew Vicent 'Dante' ametamka kuwa majeraha ya nyonga yamemtibulia mipango yote katika mechi ya juzi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Dante, juzi alipata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, lakini alijikuta akishindwa kuimaliza mechi hiyo baada ya kujitonesha nyonga dakika ya 13.

Beki huyo, mara baada ya kujitonesha katikati ya mchezo, akalala chini na kupiga ngumi ardhi kwa kuonyesha hali ya kuhuzunika. Ndiyo kwanza anaanza kupata nafasi, halafu anaumia, tena kwenye mechi kubwa namna hiyo!

Dante alisema kuwa mechi hiyo alipania kuonyesha kiwango kikubwa ili amshawishi Kocha Mkuu, Hans Pluijm lakini mipango hiyo ikapotea baada ya majeraha hayo.

Dante alisema, licha ya kupata majeraha hayo, anaamini ipo siku atapata nafasi nyingine na kumthibitishia kocha wake ubora alionao.

Aliongeza kuwa, anashukuru hivi sasa anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu huku akitarajia kuanza mazoezi leo Jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC itakayochezwa keshokutwa Jumatano.

"Nilishindwa kuendelea na mechi na kuomba kutoka baada ya kusikia maumivu makali, nitaanza mazoezi keshokutwa (leo) kama Mungu akinijalia.

"Kiukweli mechi hii ya MO Bejaia niliipania sana kucheza kwa ajili ya kumuonyeshea kocha uwezo wangu. Kiukweli roho iliniuma sana, lakini ndiyo hivyo, ninaamini kocha atanipa tena nafasi ya kucheza,” alisema Dante aliyeomba kutoka na nafasi yake ikachukuliwa na Kelvin Yondani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic