August 15, 2016



Kiungo mkabaji wa Yanga, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko, ametamba kuwa, ilikuwa lazima wawafunge MO Bejaia ya Algeria ili wafufue matumaini kwa mashabiki wa timu yao ya kufuzu kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga juzi Jumamosi ilirejesha matumaini ya timu hiyo kufuzu kucheza hatua hiyo, baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bejaia mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Lakini kesho yake ambayo ni jana Medeama ikafunga Mazembe kwa mabao 3-2.

Imepata ushindi huo kupitia kwa mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe aliyemalizia pasi ya kichwa kilichopigwa na Simon Msuva. Alifunga baada ya mabeki kujichanganya katika kuokoa.

Kamusoko aliwataka mashabiki wa timu hiyo kutokata tamaa na badala yake kuungana kwa pamoja na wachezaji wao kwa ajili ya kuwasapoti ili kufanikisha malengo yao.

“Kitu tulichokuwa tunakihitaji ni ushindi mechi hii ya MO Bejaia ambacho tumekitimiza kwa kuwafunga bao 1-0, hayo ndiyo yalikuwa mategemeo yetu kiukweli.

“Matokeo haya ya ushindi, yatatusaidia wachezaji kujenga hali ya kujiamini ndani ya uwanja, kikubwa tuliingia uwanjani kwa ajili ya ushindi, tunajua mashabiki wa Yanga walikuwa wakihitaji ushindi ili waone timu yao ikicheza nusu fainali ya michuano hii.


"Siku zote ukifanya vibaya muombe Mungu na hata ukifanya vizuri muombe Mungu kwa sababu yeye ndiye anajua kila kitu, hivyo mashabiki tuungane kwa pamoja kuhakikisha tunafuzu kucheza nusu fainali baada ya ushindi huo na MO Bejaia," alisema Kamusoko.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic