August 15, 2016

NIYONZIMA

Kiungo mchezeshaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, ameweka bayana kuwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na wapinzani wao Simba kuwa na kikosi imara huku wakiwa na straika hatari, Mrundi, Laudit Mavugo.

Niyonzima amesema kuwa msimu huu wa ligi ambao utaanza Agosti 20, mwaka huu utakuwa mgumu kuliko ule wa msimu uliopita kwa sababu timu pinzani zimefanya usajili mzuri, hasa Simba ambayo imemnasa Mavugo.

“Mavugo namjua na niliwahi kucheza naye zamani, kwa hapa Simba wamepata bonge la straika kwani jamaa ni mzuri zaidi katika kufunga na hakika kwa msimu huu mambo yatakuwa magumu zaidi.

MAVUGO
“Kikubwa ambacho tunatakiwa kukifanya ni kujiandaa zaidi kwani kama tukifanya makosa yoyote, mambo yanaweza kuwa mabaya kwa upande wetu kutokana na wenzetu kuwa na uchu na ubingwa,” alisema Niyonzima.    

Mavugo tangu atue hapa nchini, amefanikiwa kuandika rekodi ya pekee ambayo haijawahi kutokea hapa nchini na kujikuta akiwafunika Donald Ngoma na Amissi Tambwe walioipa jeuri Yanga msimu uliopita.

Rekodi hiyo ambayo Mavugo amefanikiwa kuiandika katika kipindi cha wiki mbili akiwa hapa nchini, ni ile ya kuushawishi uongozi wa Simba na kujikuta ukianza mikakati ya kutaka kumuongezea mkataba mwingine wa miaka miwili, ikiwa ni siku chache tu baada ya kusaini mkataba mwingine kama huo, jambo ambalo Ngoma na Tambwe hawakuweza kulifanya.

Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema: “Taarifa hizo bado hazijanifikia mezani kwangu lakini kama ni kweli basi siyo jambo baya, ni jambo zuri kwani Mavugo siyo mchezaji wa kawaida, kiwango chake ni cha Ulaya na siyo cha Afrika, hivyo itakuwa vizuri kama uongozi una mpango huo.”0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV