August 6, 2016Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amekata kiu ya kile ambacho wanachama wengi na wapenda soka nchini walikuwa wakikisubiri kwenye mkutano wa dharura aliouitisha.

Baada ya kujadili, wanachama wa Yanga pamoja na wajumbe wa bodi wakapitisha kumkodisha Manji kwa miaka kumi kama alivyoomba.

Katika mkutano huo unaofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kipindi hiki, Manji amesema amepeleka ombi la kuikodisha Yanga kwa miaka 10.

“Nitaikodisha kwa asilimia 75 na 25 inabaki kwa wanachama. Nataka kuikodisha timu na nembo, majengo ya klabu yanabaki kuwa mali ya wanachama.

“Katika miaka 10, ikipatikana faida 25 inakwenda kwa wanachama na klabu na 75 kwangu. Kama itakuwa ni hasara basi inakuwa hasara yangu, hakuna hasara upande wa wanachama au klabu,” alisema.

“Tayari nimewasilisha ombi hilo Bodi ya Wadhamini ambao wao watazungumza na nyinyi wanachama na kama kutakuwa na makubaliano basi tutaingia mkataba,” alisema Manji.


Manji alisema masuala ya timu kuhusu usajili, mishahara, uendeshaji kama safari na gharama nyingine zitakuwa chini yake.

Pia asilimia 25 ambayo itakuwa ni ya klabu, ndiyo itatumika kuujenga Uwanja wa Kaunda na Yanga itakuwa na uwanja wa kufanyia mazoezi na ikiwezekana hata kuchezea mechi.

Wanachama wengi walionekana kufurahi na wengi walisisitiza kwamba wanakubali hata kabla ya kuanza kwa mchakato huo rasmi.

3 COMMENTS:

 1. Manji hana pesa ya kumiliki timu MANJI anajulikana mwisho kigoma alafu amkejeli mtu anaye julikana Dunia nzima, mwenzake anaacha Ubunge yeye anagombea Udiwani, huwezi kushindana na aliyekuzidi, mwenzake anawekeza Yeye Hakodi anaiazima jiulize anaikodi Kwa kiasi gani Hasemi, ndio maana alijua akiwaambia Ajenda mapema wanayanga wafikiri marambili wangepinga ndio maana amewastukiza AJENDA ndani ya kikao, na wanayanga bila kuelewa wakakubali, manji klabu anaitaka bure pamoja na nembo yake, alafu faida achukue 75% na wanachama na club ni 25%, wakati MO anaweka 20 bilion faida yote inabaki kwenye club, Wanayanga jifikilieni kwanza alafu mtupe jibu MO na Manji nani anataka kuitumia club kujinufaisha?

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hauna jipya!Manji anataka kutumia chapa ya Yanga kisha asilimia 25 ya faida inarudi klabuni, wewe unayejiona mjanja unabariki kuuza zaidi ya nusu ya asset za Simba kwa pesa itakayokwenda kwny treasury bonds...Mbumbumbu atabaki kuwa mbumbumbu miaka mia...Rage was right...

   Delete
 2. Uwezo wa kufikiri unapotawaliwa na ushabiki. Hamna point zinazoweza kujenga. Intergent people talk because they have something to say but fools talk because they have to say something. No offence

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV