Saa chache baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva kushikiliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), kumeibuka sababu kadhaa ambazo zinazungumzwa kuwa ni chanzo.
Taarifa zinaelezwa kuwa Takukuru wanamshikilia Aveva kwa tuhuma za rushwa ingawa haijaelezwa ni tuhuma zipi.
Kumekuwa na taarifa ambazo si rasmi kuwa Aveva aliingiza fedha za Okwi zaidi ya Sh milioni 450 kwenye akaunti yake binafsi kuhofia zichukuliwe na TRA kwa kuwa Simba inadaiwa.
Simba inadaiwa zaidi ya Sh milioni 650, hali hiyo imesababisha kuonekana kama vile alikuwa akikwepa kodi.
Malipo ya fedha hizo, zaidi ya Sh milioni 450 ni malipo ya ununuzi wa mshambuliaji Emmanuel Okwi ambazo Simba ilimuuza katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Taarifa hizo zimeeleza kwamba waliamua kuzificha ili waweze kujenga uwanja wao wa Bunju ambao tayari walianza kuujenga .
Lakini kuna baadhi wamekuwa wakieleza kwamba Aveva ana kisa na mtu nje ya hapo ambaye ‘amemchoma’.
Hata hivyo, kwa kuwa Takukuru bado wanaendelea na uchunguzi na suala lake ni tuhuma, uchunguzi utakapokamilika, wao ndiyo wataeleza ukweli tupu kuhusiana na suala hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment