August 7, 2016


WAKIWA NA TORRES..

Watoto kadhaa kutoka nchini Rwanda wamefanya ziara ya mafunzo ya soka nchini Hispania na kubahatika kushuhudia mazoezi ya Atletico Madrid.

Watoto hao wamefanya ziara hiyo ya mafunzo kupitia kampuni ya RG Consultant and Sports Solution ya nchini humo na walipokelewa na mshambuliaji nyota wa Atletico Madrid, Fernando Torres ambaye pia aliwahi kung'ara na Liverpool.

WAKIWA NA GARCIA, WAKISHUHUDIA MAZOEZI YA ATLETICO MADRID CHINI YA DIEGO SIMEONE.
Torres aliwaonyesha upendo na watoto hao walionekana kuwa ni wenye furaha kuu wakati wakipiga naye picha.

Mkurugenzi wa RG Consultant and Sports Solution, Rayco Garcia amesema watoto hao bado wako nchini Hispania na wataendelea na mafunzo ya soka kwa lengo la kukuza vipaji vyao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV