August 25, 2016Kikosi cha Ruvu Shooting kipo tayari kuiangusha Prisons ya Mbeya Jumamosi na kinataka kufanya hivyo ili iwe dawa ya kuimaliza Simba!

Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kwa kuwa walianza ligi na ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar, amesema wanataka kuendeleza ushindi huo ili waimalize Simba.

“Kama tukishinda mechi ya Jumamosi dhidi ya Prisons pale Mbeya, basi morali itakuwa juu, ninaamini Simba atakwenda na maji.

“Tunataka kuwa timu ya kwanza kuitia doa, maana watu wanaiamini sana. Wanasema safari hii iko vizuri. Sasa tunataka kuwaonyesha tuko vizuri zaidi.

“Ndiyo maana tunataka kuiangusha Prisons kwanza ili kujiweka vizuri wakati tukiisubiri Simba mechi inayofuata,” alisema Masau.

Tayari kikosi cha Ruvu Shooting kimeanza safari kwenda Mbeya kuwavaa Prisons ambao pia walianza ligi kwa ushindi wa bao 1-0 wakiwa ugenini mjini Songea dhidi ya Majimaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV