Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ametuma rambirambi kwa kipa wake Deougratius Munish ‘Dida’ kutokana na msiba alioupata wa kufiwa na baba yake mzazi.
Dida amepatwa na msiba huo wakati akiitumikia Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Pluijm ameandika kwenye akaunti yake ya Facebook akimtakia Dida uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kufiwa na baba yake mzazi.
Kama haitoshi, kocha huyo akaweka picha akiwa na Dida hospitalini walipokwenda kumuangalia mzee wake huyo wakati amelazwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment