August 12, 2016


Mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, ameweka wazi kuwa licha ya kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa Simba Day lakini bado anajipanga kwa kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kuipa mataji zaidi, hasa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao unashikiliwa na wapinzani wao Yanga.

Mavugo amejiunga na Simba hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Vital’O ya Burundi, licha ya kucheza katika mchezo mmoja wa timu hiyo, ameweza kuwakosha mashabiki wa timu hiyo kutokana na kiwango cha hali ya juu alichokionyesha kwenye mchezo wa timu hiyo dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.

Mavugo alisema anatoa ahadi hiyo ya kujituma na kuipa makombe Simba kutokana na viongozi kuonyesha uungwana kwa kumvumilia kwa kipindi cha msimu mzima ambapo alitarajia kujiunga na timu hiyo tangu msimu uliopita.

“Nina deni kubwa sana hapa Simba ambalo kwa namna yoyote natakiwa kulilipa kwa kuwapa mafanikio ikiwepo ya kutwaa mataji kwa sababu viongozi wake walinionyesha kitendo cha uungwana katika msimu uliopita ambapo nilitakiwa kuja na sikuja.

“Hiyo ni dalili ya heshima waliyonipa kwa upande wangu, hivyo sina namna nyingine ya kuilipa zaidi ya kuwapa makombe lakini hilo litatimia endapo nitapata ushirikiano kikamilifu kutoka kwa wachezaji wengine wa hapa,” alisema Mavugo.  


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic