August 16, 2016


Mshambuliaji mstaafu wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema bado ana nafasi kubwa ya kutoa msaada ndani ya kikosi chake.

Mgosi amesema ataendelea kutoa msaada ili kuhakikisha Simba inafanya vizuri kwa kuwa yuko katika benchi la ufundi.

“Watu wa benchi la ufundi wanapigana kabisa kama mchezaji, wanakuwa katika kupanga mbinu, kusaidia wachezaji na kwa ujumla kuisaidia timu.

“Mimi niko kwenye benchi la ufundi, hivyo nina nafasi kubwa ya kutaka kuona Simba inafanya vizuri safari hii nikiwa meneja,” alisema Mgosi.


Mgosi ametangaza kustaafu soka na baadaye akaagwa wakati Simba ikicheza mechi yake ya kirafiki dhidi ya URA ya Uganda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV