August 14, 2016


Nahodha wa Simba, Mussa Hassan Mgosi aliyetangaza kustaafu amesema asingesubiri hadi ifikie mashabiki waanze kumzomea.

Amesema aliamua kustaafu akiwa anaheshimika, anahitajika na ndiyo maana amefurahi kuondoka katika kipindi hiki.

“Nimeondoka katika kipindi ninahitajika, ninafurahi kwa kuwa bado nitaendelea kubaki ndani ya kikosi cha Simba na kutoa msaada wangu,” alisema.

“Bora kuondoka mapema wakati unahitajika kuliko kusubiri kipindi cha malumbano, au mashabikikuanza kulalamikia.”

“Niwashukuru sana Wanasimba wote kwa ushirikiano wao, naomba waiunge mkono timu yao katika kipindi kigumu au kile cha furaha,” alisisitiza.

Mgosi sasa anachukua nafasi ya Meneja wa kikosi cha Simba na ataendelea kushirikiana na wachezaji.


Mgosi alipata nafasi ya kuichezea timu hiyo mara ya mwisho katika kikosi hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV