August 14, 2016


Liverpool imeionyesha Arsenal si kitu kwake baada ya kuichapa mabao 4-3 licha ya Arsenal kuwa nyumbani Emirates tena ikianza kufunga.

Arsenal ilikuwa ya kwanza kufunga bao kupitia kwa Theo Walcott dakika ya 30, ambaye muda mchache alikosa mkwaju wa penalti. Dakika ya 45, Coutinho akasawazisha.

Adam Lallana akafunga dakika ya 49 huku Coutinho akiongeza bao la tatu dakika ya 56.


Arsenal walianza kujipanga lakini kabla hawajakaa vizuri, Sadio Mane akafunga bao la nne katika dakika ya 63 na kuwalazimu Arsenal kuongeza juhudi hadi walipopata bao la pili katika dakika ya 64 kupitia Oxlade Chamberlain.

Katika mechi hiyo ya ufunguzi wa Ligi Kuu England, Arsenal iliongeza bao la tatu katika dakika 75 kupitia Calum Chambers katika dakika ya 75 lakini ikashindwa kupata bao la kusawazisha kwa dakika 25 zote za mwisho.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV