August 1, 2016


Simba imeendeleza dozi katika mechi zake za kirafiki baada yakuichapa Burkina Faso ya Morogoro kwa mabao 5-0.

Katika mechi hiyo ya kirafiki, Ibrahim Ajib ameendelea kung’ara baada ya kufunga mabao mawili huku Moussa Ndusha raia wa DR Congo, Shiza Kichuya na Said Ndemla kila mmoja akitupia moja.

Hii ni mechi ya tatu ya Simba ya kirafiki na zote imeshinda ikianza na ile dhidi ya Polisi Moro iliyoshinda 6-0 kabla ya kuitwanga Moro Kids 2-0.


1 COMMENTS:

  1. Mmekuwa wazee wa kugawa dozi lakini timu zenyewe mmmh!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV