August 12, 2016


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema limefikisha kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), utetezi wa timu zote zilizoshindwa kuwasilisha usajili wao hadi dirisha linafungwa.

Moja ya timu zilizoshindwa kufanya hivyo kwa mujibu wa TFF ni Yanga na imetoa taarifa mambo mawili yanaweza kutokea.

TFF imesema kati ya mambo mawili yanayoweza kutokea ni timu hizo kuteremshwa hadi daraja la chini kabisa au la tatu au kutozwa faini ya dola 500 kwa kila mchezaji kama dirisha litafunguliwa.


“Hivyo Fifa haijatoa majibu hadi sasa, lakini kama itakuwa ni majibu lazima kati ya hayo mawili,” alisema Alfred Lucas Mapunda ambaye ni msemaji wa TFF.

TFF imesema ilifanya kazi ya kufikisha utetezi wa klabu ambazo hazikufanya usajili kwa wakati mwafaka na moja wapo ni Coastal Union.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV