August 7, 2016


Hivi karibuni mmiliki wa Leicester City, alitoa magari kwa kila mchezaji wa kikosi hicho baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa England.

 Vichai Srivaddhanaprabha aliwapa wachezaji wake kila mmoja gari aina ya  BMW I8s, thamani ya gari moja ni pauni 105,000. Magari hayo yanatumia umeme.


Pamoja na kuonekana ni kama kitu, imeelezwa kwa Ujerumani wala si jambo geni kwani tokea mwaka 2002, wachezaji wa Bayern Munich wamekuwa wakipewa kila mmoja gari jipya kila msimu.

Magari hayo aina ya Audi ambao ni wadhamini wa Bayern Munich, yamekuwa yakitolewa kila kitu cha majira ya joto, mara moja kwa msimu bila ya kujali wamekuwa mabingwa au la.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV