August 10, 2016


Kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Mhispania, Zeben Hernandez, keshokutwa Ijumaa kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mamlaka ya Kodi Uganda (URA) ya Uganda kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo kwa Azam utakuwa ni wa nane wa kirafiki katika maandalizi yao ya kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 20, mwaka huu.

Ofisa Habari wa Azam, Jafar Idd, ameliambia gazeti hili kuwa, wanatarajia kucheza mchezo huo wa kirafiki ili kukipima zaidi kikosi chao baada ya kucheza na timu za hapa nyumbani.

“Ijumaa tunatarajia kucheza na URA ya Uganda katika muendelezo wa mechi zetu za kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu ujao, kila baada ya mchezo mmoja kumalizika, mwalimu na benchi lake la ufundi huwa wanaangalia wapi kuna kasoro ili wazifanyie kazi mapema kabla ya kuanza kwa msimu.


“Kwa jinsi matokeo tuliyoyapata kwenye mechi zilizopita, ni ishara kikosi kipo kwenye mazingira mazuri ya kuanza kupambana kuwania taji la ligi kuu,” alisema Idd.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV