August 4, 2016Taarifa zinaeleza, wajumbe wengine wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba nao wameitwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Inaelezwa, wajumbe hao wa kamati ya utendaji nao wanahojiwa kuhusiana na tuhuma za fedha wakiwa pamoja na Rais wa Simba, Evans Aveva.

Aveva alishikiliwa tokea jana na kulala katika kituo cha Polisi cha Urafiki jijini Dar es Salaam na leo mchana alipelekwa kwenye makao makuu ya Takukuru enero la Upanga kwa ajili ya mahojiano zaidi.


Taarifa zinasema wajumbe hao wa kamati ya utendaji nao wamekuwa wakihojiwa na tuhuma ni zilezile zilizoelezwa kumgusa Aveva kuhusiana na fedha za malipo ya Emmanuel Okwi kuhamishiwa kwenye akaunti yake.

1 COMMENTS:

  1. habari haijakamilika, yaani hao watatu ni akina nani

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV