September 21, 2016


Kama unakumbuka, Salehjembe ilikuwa blog ya kwanza kukueleza mshambuliaji wa Mrisho Ngassa amepaa kwenda Oman kujiunga na Fanja FC

Sasa Ngassa amemalizana na Fanja kwa kusaini mkataba wa miaka miwili, leo.

Wakati Ngassa aliyevunja mkataba na Free State Stars ya Afrika Kusini akimalizana na Fanja FC, tayari klabu hiyo ilishamsajili Danny Lyanga kutoka Simba.


Lyanga amejiunga na Fanja rasmi baada ya kufuzu majaribio na kupewa mkataba wa miaka miwili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV