September 21, 2016


Uwanja wa Uhuru hautatumika katika mechi kadhaa za Ligi Kuu Bara.

Hii ni kutokana na marekebisho na utalazimika kufungwa tena kwa muda huku baadhi ya mechi zikirejea kwenye Uwanja wa Taifa.

Mechi mbili za raundi ya sita za Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Majimaji na African Lyon dhidi ya Kagera Sugar zitapigwa Taifa.


Baada ya maoni ya baadhi ya wadau na Simba kupeleka maombi ya kulalamika kuhusiana na uwanja huo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeamua kuufunga kwa muda ili ufanyiwe marekebisho hasa katika nyasi bandia ambazo zimeelezwa kungandana na mipira midogo na kuufanya kuwa mgumu na hatari kwa afya za wachezaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV