September 21, 2016


MAHADHI
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi amemtabiria makubwa mshambuliaji wa timu hiyo, Mrundi, Amiss Tambwe, kuwa endapo hatapatwa na majeraha basi anaweza kutetea tuzo yake ya ufungaji bora na kumfunika vibaya Mrundi mwenzake wa Simba, Laudit Mavugo.

Mahadhi ameliambia Championi Jumatano kuwa Tambwe ni mchezaji asiyetabirika uwanjani kwani ana uwezo mkubwa na kufunga muda wowote ule kwa kutumia viungo vyake vyote, tofauti na washambuliaji wengine.

“Hata ukizungumza na mabeki wa timu nyingine watakwambia kuwa Tambwe ni mshambuliaji asiyetabirika, utamkaba sana lakini ukijisahau kidogo lazima akauumize na anajua kuzitumia vilivyo nafasi anazopata.


TAMBWE (KULIA).

“Katika mechi anaweza kupata nafasi tatu hivyo katika hizo lazima moja atafunga hivyo namtabiria kuwa anaweza kutetea nafasi tuzo yake hivyo ambayo hata mimi naitamani lakini kusema kweli siwezi kushindana naye,” alisema Mahadhi.


Tambwe kwa sasa ameshazifumania nyavu mara tatu katika mechi nne alizoitumikia timu hiyo msimu huu sawa na Mavugo, John Bocco (Azam), Hood Mayanja (African Lyon), Rafael Daud (Mbeya City) na Adrahman Mussa (Ruvu Shooting).

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV