Beki wa Manchester United, Chris Smalling, usiku wa jana alilazimika kupata msaada wa polisi wakati akielekea uwanja wa ndege baada ya mchezo wa timu yake dhidi ya Feyenoord katika Europa League nchini Uholanzi.
Smalling alijikuta katika hali hiyo baada ya kutakiwa kufanyiwa vipimo kuona kama anatumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.
Kocha wa Man United, Jose Mourinho na kikosi cha wachezaji wa timu hiyo waliondoka kwenye vyumba vya Uwanja wa De Kuip na kumuacha Smalling ambaye yeye na mchezaji mwingine wa United, Ander Herrera walichaguliwa kufanyiwa vipimo hivyo.
Kawaida ya Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) ambalo ndilo linalosimamia michuano hiyo, limekuwa likiwahukua wachezaji ambao wanatiliwa mashaka au wanaweza kuchagua tu yeyote ili kumfanyia vipimo hivyo.
Baada ya kuchelewa kumaliza zoezi hilo la kutoa haja ndogo, Smalling alilazimika kupata kampani hiyo ya askari kwa kuwa tofauti na hapo angechelewa ndege iliyokuwa ikimsubiri.
Askari aliyehusika kumsindikiza uwanjani wa ndege aliweka picha kwenye mtandao na kuandika kuwa amekamilisha zoezi la kumuwahisha Smalling uwanjani hapo baada ya kuchelewa kutoa haja ndogo wakati wa upimwaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment