September 11, 2016

NA SALEH ALLY, BARCELONA
Unaweza kusema kuwa dharau za Kocha  Luis Enrique zinaweza kuwa zimewaponza Barcelona ambao wameambulia kipigo cha mabao 2-1 wakiwa nyumbani kutoka katika timu ndogo ya Alaves katika La Liga.
 

 
Barcelona ambayo imepata kipigo hicho cha kwanza msimu huu tena ikiwa nyumbani kwake kwenye Uwanja wa Camp Nou ilianza mchezo huo bila kuwa na mastaa wake watatu Iniesta, Luis Suarez na Lionel Messi ambao walikuwa kwenye benchi.

Licha ya baadaye kuwaingia mastaa hao kipindi cha pili bado hawakuweza kubadili au kuichagiza timu yao kupata ushindi wala kusawazisha jambo ambalo limewafanya wengi kupatwa na mshtuko kwa kuwa ni matokeo ambayo yalikuwa hayategemewi.Matokeo hayo ni mabaya kwa Barcelona kwa kuwa wapinzani wao wa jadi, Real Madrid walipata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Osasuna, hivyo wanaongoza ligi wakiwa na pointi 9 wakati Barcelona wamebaki na pointi zao sita.

Katika mchezo huo ambao pia ulikuwa wa kwanza kwa kipa mpya wa Barcelona, Jasper Cillenssen, bao lao lilifungwa na beki Mathieu katika dakika ya 46 wakati mabao ya ‘madogo’ hao yalifungwa na Deyverson (39) na Gomez (64).

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV