September 11, 2016

Unaposikia derby katika soka lazima ukubali kuwa mechi za aina hiyo siyo mchezo, wakati Manchester City ikiitoa nishai Manchester United kwa kuifunga mabao 2-1 kwenye Uwanja wa  Old Trafford katika Manchester  Derby, kuna beki mkoja ameondoka na alama ya milele.

  Beki wa Man City, Aleksandar Kolarov amejikuta akiacha jino lake moja kwenye nyasi za uwanja huo kutokana na purukushani zilizokuwa zikitokea uwanjani japokuwa aliondoka akiwa na furaha. 


  Katika mchezo huo ambapo mabao ya washindi yalifungwa na Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho huku lile la United likiwekwa wavuni na Zlatan Ibrahimovic, Kolarov alikuwa akipambana mara nyingi na kiungo wa Man United, Marouane Fellaini.

Mara baada ya mchezo huo, kipa wa pili wa Man City, Willy Caballero alitupua picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa na Kolarov ambaye alikuwa akitabasamu huku akiwa na pengo sehemu ya kulia ya kinywa chake.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV