September 16, 2016

Nahodha na beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema amezisikia tambo za watani wao wa jadi, Simba, lakini akawaambia: “Simba wana pointi zetu sita tena kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara.”

Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni mara baada ya kupata taarifa za Simba kutamba kuwafunga Oktoba Mosi, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Cannavaro alisema anapata matumaini ya kuwafunga Simba kutokana na ubora wa kikosi chao kinachoundwa na wachezaji wengi wenye uzoefu wa kimataifa.

“Tumepanga kuweka rekodi kubwa kwenye msimu huu wa ligi kuu, moja kabisa kuutetea ubingwa pia kufunga kila mechi tutakayocheza ikiwemo hiyo ya Simba.

“Ninajua Simba wanapata matumaini ya kutufunga kutokana na usajili wao wa hivi karibuni lakini hiyo kwangu wala hainipi hofu, ninaamini sisi ni bora zaidi yao, ndiyo maana tumefika hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Tutawafunga katika mechi zote mbili, niamini katika hilo,” alisema Cannavaro.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV