September 14, 2016

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho, amemaliza mazungumzo na uongozi wa timu hiyo na juzi alfajiri alirejea kwao huku akiwa na siri nzito moyoni.

Mbrazili huyo, alitua nchini Jumatano iliyopita huku akificha sababu za kuitwa na uongozi wa Yanga kabla ya Jumapili alfajiri kurejea kwao Brazil.Kiungo huyo aliondoka Yanga baada ya kusitishiwa mkataba wake wa mwaka mmoja kabla na kutimkia Rakhine United FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Myanmar.Akizungumza na Championi Jumatano, Coutinho alisema ni ngumu kwake hivi sasa kuweka wazi mazungumzo aliyofanya na uongozi wa timu hiyo, kwani ni siri kati yake na mabosi wake.

Coutinho alisema, kikubwa anachoweza kukiongea ni kwamba yupo tayari wakati wowote kurudi kuichezea Yanga pale watakapohitaji huduma yake ya ndani ya uwanja.

“Mimi niliondoka Yanga kwa amani bila ya kugombana na mtu, kiukweli niliishi kwa amani na ushirikiano mzuri kwa kuanzia kwa wachezaji, kocha na viongozi.

"Kama Mungu akipenda nitarejea tena kuichezea Yanga kama wakinihitaji kwa ajili ya kuichezea timu hiyo, kiukweli Yanga ni moja ya klabu ninazopenda kuzichezea kutoka moyoni.

"Pia ukubwa wenyewe wa timu inayoundwa na wachezaji wa mataifa kutoka nchi mbalimbali na ushiriki wao wa michuano ya kimataifa ambayo mwaka huu ilifika hatua ya Nane Bora Afrika, lakini kwa suala la ishu tuliyoongea naomba nibaki nayo moyoni," alisema  Coutinho.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV