September 13, 2016

Nyota wa soka aliyewahi kutamba katika timu ya Barcelona, PSG, AC Milan na timu ya taifa ya Brazil amesema kuwa anatarajia kustaafu kucheza soka rasmi mwishoni mwa msimu huu ikiwa ni miaka 18 tangu aanze kucheza mchezo huo katika Bara la Amerika ya Kusini na Ulaya.
 
Staa huyo ni Ronaldinho Gaucho ambaye amesema kuwa kwa umri wa miaka 36, anahisi mwili wake unahitaji kupumzika na sasa yeye siyo kijana wa miaka 26, hivyo hata kasi yake uwanjani imepungua.

Ronaldinho, mmoja wa wachezaji walioonyesha uwezo wa juu kwa kucheza soka la kuvutia alianza kuwa staa wa dunia mara baada ya kutua Barcelona mwaka 2003 ambapo alikuwa sehemu ya mchango wa mabadiliko ya ltimu hiyo kuwa bora Ulaya na duniani kwa kumla.

“Naangalia nini cha kufanya nimalizie maisha yangu ya soka, plani iliyopo ni kucheza kwa mwaka moja, kisha nitastaafu, nitaelekeza nguvu katika miradi mingine kama muziki,” alisema mchezaji huyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV