September 13, 2016

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, El-Hadji Diouf amesema kuwa alimwambia Mario Balotelli kuhusu nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard atamfanya awe na maisha magumu klabuni hapo na kumshauri kutojiunga nao.


Balotelli ambaye ameondoka Liverpool akiwa hana mafanikio, juzi alinukuliwa akisema kuwa anajutia kujiunga na Liverpool na ndiyo uamuzi mbaya aliowahi kuufanya katika maisha yake. Kwa sasa yupo Nice ya Ufaransa.


 “Nilimwambia kutokwenda Liverpool. Nilimwambia  Gerrard hatapenda mchezaji awe juu yake,” alisema Diouf na kuongeza:

“Gerrard ni mtu mwenye wivu sana na ambaye hapendi maendeleo ya wengine. Mario ni mtu safi sana na unatakiwa kumsikiliza, siyo mtu ambaye anaweza kuvuruga mambo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

“Kuna vitu vingi vimetengenezwa juu yake, lakini mengi yanayoongewa juu yake ni upuuzi tu.

“Alipotua England alikuwa bado kijana mdogo unatakiwa kulijua hilo, alipewa presha kubwa sana.”

Diouf na Gerrard walikuwa pamoja Liverpool lakini hawakuwahi kuelewana na hata baada ya Diouf kuondoka klabuni hapo wawili hao wameendelea kurushiana vijembe lakini zaidi ni Msengali huyo ndiye ambaye amekuwa akizungumza mara nyingi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV