September 13, 2016

Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limeikabidhi Azam FC ngao ya jamii ambayo ni halisi baada ya awali kupewa ngao ‘feki’ mara baada ya kuifunga Yanga kwa penalti wakati wa ufunguzi wa msimu huu wa 2016/17.

Mara baada ya kukabidhiwa ngao feki, wachezaji wa Azam walishangaa kuona karatasi lililokuwa na maandishi likinyofoka na hivyo kuwa na kazi ya kuliweka vizuri wakiwa hapohapo uwanjani.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba  ndiye ambaye alipokea ngao hiyo kwa niaba ya klabu yake, ambapo kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, ngao hiyo mpya ni sehemu ya vifaa kadhaa vilivyotua nchini vikitokea China.


“Siyo ngao tu kuna vifaa vingine vya TFF vilivyotua nchini na ndiyo maana awali tuliwakabidhi ile ngao kwa kuwa hii ya sasa ilichelewa. Pia kuna ngao za misimu mitano mfululizo zimetua katika hivyo vifaa,” alisema Alfred.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV