September 13, 2016

Mchezo wa Manchester City dhidi ya Borussia Monchengladbach uliokuwa umepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Etihad, usiku wa Jumanne Septemba 13, 2016 umeahirishwa kutokana na mvua na hali ya hewa kutokuwa nzuri.

Shirikisho la Soka la Soka la Ulaya (UEFA) limefikia uamuzi huo kutokana na wakaguzi wake kutoa uamuzi huo baada ya kuukagua.Mchezo huo ulikuwa ni wa kwanza katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, ikielezwa kuwa kipa wa Man City, Claudio Bravo alishauriwa kutofanya mazoezi katika uwanja huo kutokana na uwanja kutokuwa katika hali nzuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV