September 17, 2016

Beki wa kati wa Simba, Juuko Murshid, amerejea mzigoni lakini amekumbwa na gonjwa la ajabu, hivyo ametengewa ratiba maalumu ya mazoezi tofauti na wenzake ili arudi katika hali ya kawaida.

Juuko aliyekuwa kwao Uganda ambako alienda kuchezea timu ya taifa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika, alijiunga na Simba Jumamosi iliyopita baada ya kumaliza majukumu yake.


Hata hivyo, Juuko amerejea akiwa na tatizo la ugonjwa wa mba kichwani ambalo limemfanya kuvimba sehemu ya ngozi yake kichwani, pia anashindwa hata kupiga mipira ya kichwa.

Kocha wa Simba, Joseph Omog, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, amefurahi kurejea kwa Juuko lakini amesikitika kuona amerejea akiwa na ugonjwa huo sehemu ya kichwani.


“Ana matatizo kidogo sehemu ya kichwa, alipokuja alikuwa hawezi hata kupiga mpira kwa kichwa maana anaumia. Anasumbuliwa na kitu kama mba,” alisema Omog.

Kwa mujibu wa Juuko mwenyewe, ili apone tatizo hilo ametakiwa kukimbia umbali mrefu ili kupata jasho kichwani ambalo linasaidia kupunguza mba.

Juzi Alhamisi, Championi Jumamosi lilimshuhudia Juuko akikimbia pembezoni mwa Barabara ya Ununio inayopita jirani nia Uwanja wa Boko Veterani unaotumiwa na Simba kwa mazoezi.

 “Hii programu niliyonayo kwa sasa ni pamoja na mazoezi ya mpira lakini zaidi kuutibu huu ugonjwa wa mba, umekuwa mkubwa kama unavyoona mpaka nimevimba hadi nje ya nywele, ulikuwa unakuja usoni.

 “Kinachotakiwa ni kutokwa sana na jasho kichwani ili liguse mba, maana ukipata jasho inawasha na sitakiwi kugusa maana ndiyo napona,” alisema Juuko.

Ugonjwa wa mba wa kawaida humfanya mgonjwa kutokwa na ukoko au vumbi kichwani, lakini huu wa Juuko humemfanya avimbe na kupata maumivu makali.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic