September 14, 2016

KICHUYA

Winga wa Simba, Shiza Kichuya, amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuzungumza na waamuzi ili wamlinde pindi anapokuwa uwanjani.

Kichuya ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea Mtibwa Sugar, amefikia hatua hiyo baada ya kudai kuwa baadhi ya mabeki wa timu pinzani, hawana nia nzuri naye kwenye kila mechi anayocheza.

Kichuya alisema kuwa tangu aanze kuitumikia Simba msimu huu, amekuwa akikumbana na changamoto mbalimbali kutoka kwa mabeki wa timu pinzani ambao wamekuwa wakimchezea faulo za ajabu zinazoweza kumsababishia majeraha, hivyo akashindwa kuendelea na majukumu yake ya kuitumikia klabu yake hiyo.

“Nawaomba TFF wakae na waamuzi ili wawaambie waweze kunilinda, vinginevyo nitaumizwa vibaya.

“Mabeki hivi sasa wananikamia sana na wamekuwa wakinichezea faulo za ajabu hata kama ndiyo njia ya kunipunguza makali siyo hivyo, wanaweza kuniumiza nawaomba TFF wanilinde,” alisema Kichuya.

SOURCE: CHAMPIONI


1 COMMENTS:

  1. Mbona wenzie hawalalamiki au ndio kashajiona nyota!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV