September 13, 2016

Arsenal imetoshana nguvu na Paris Saint-Germain (PSG) katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Arsenal imekutana na ugumu huo katika mechi ya ufunguzi hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya  kwenye Uwanja wa Parc des Princes usiku wa kuamkia leo jijini Paris Ufaransa.
  Katika mchezo huo wa Kundi A ulikuwa wa kasi kwa timu zote hasa kipindi cha kwanza ambapo Edinson Cavani alifunga bao la PSG katika dakika ya kwanza tu ya mchezo huo baada ya mabeki wa Arsenal kujisahau wakati lile la kusawazisha liliwekwa wavuni na Alexis Sanchez katika dakika ya 78.
 PSG walikuwa wakali kipindi cha pili lakini Cavan alishindwa kutumia nafasi nyingi alizopata kuanzia kipindi cha kwanza hadi cha pili.

Katika mchezo huo beki wa PSG, Marco Verratti na straika wa Arsenal, Olivier Giroud wote walipata kadi nyekundu katika dakika ya 90 kutokana na kuonyeshana mchezo mbaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV