September 20, 2016


Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez ameeleza wazi kwamba mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu alikuwa tatizo kwenye safu yake ya ulinzi walipopoteza bao 1-0 dhidi ya Simba.

Lakini akasisitiza kikosi chake kilicheza vizuri zaidi lakini hawakuzitumia nafasi za kufunga.

ZEBEN (KULIA) AKISALIMIANA NA OMOG

Katika mechi hiyo, Azam FC kweli ilionyesha kiwango kizuri na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.

“Simba waliitumia nafasi waliyopata na kutumaliza. Ajib alikuwa tatizo lakini walimdhibiti,” alisema.

Mechi hiyo ilitawaliwa na mashambulizi ya zamu ingawa Azam FC walionyesha wakishambulia zaidi hasa kipindi cha kwanza.


Kipigo cha Simba, inakuwa mechi ya kwanza Azam FC kupoteza msimu huu chini ya Mhispania huyo kijana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV