September 20, 2016


Kuna kila dalili, Simba itataka kumlinda mchezaji wake Ibrahim Ajibu asipate kadi ya tatu ya njano.

Ajibu ana kadi mbili za njano na benchi la ufundi la Simba, linaweza kujithatiti asijeze mechi ijayo dhidi ya Majimaji ili kuhakikisha anaivaa Yanga Oktoba Mosi.

“Kweli Ajibu ana kadi mbili za  njano na sisi watu wa benchi la ufundi tumeliona hili. Lakini bado utabaki kuwa uamuzi wa kocha mwenyewe (Omog),” kilieleza chanzo.

Simba inaivaa Majimaji Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya hapo Simba watakuwa kwenye maandalizi ya mechi yao dhidi ya watani wao Yanga, Jumapili inayofuatia.

Hivyo suala la tahadhari linaweza kufanya Ajibu akose mechi hiyo ili kuhakikisha anakuwepo kusaidia safu ya ushambulizi dhidi ya Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV