September 16, 2016

Yanga wapo mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi kuu Bara dhidi ya Mwadui FC, kesho Jumamosi lakini kabla ya kufika mkoani hapo safari yao ilikuwa na changamoto za hapa na pale ikiwemo wachezaji wa Yanga kupanda daladala.

Yanga waliondoka Dar es Salaam, jana asubuhi kwa ndege ya Shirika la Fast Jet, walielekea Mwanza ili wakifika hapo waunganishe na basi kwenda Shinyanga.


Wachezaji wa Yanga wakiingia kwenye gari ndogo.
 


Basi ambalo liliwapeleka Yanga mkoani Shinyanga wakitokea Mwanza.


 Baada ya kutua Mwanza wachezaji na msafara wa timu hiyo, walionekana wakizunguka zunguka uwanjani hapo, baada ya muda wachezaji wakaonekana wakiingia kwenye gari ndogo mbili za kusafirisha abiria jijini Mwanza ‘daladala’ bila kueleweka wanapoelekea.

Alipotafutwa nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuelezea kilichotokea alisema gari kubwa lililotakiwa kuwafuata kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza lilichelewa, hivyo wakapanda gari hizo ndogo kabla ya baadaye kupata gari kubwa lililowasafirisha hadi Shinyanga.

Kitendo cha Yanga kupanda daladala kilisababisha picha za tukio hilo kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii huku wale wapinzani wa Yanga wakionekana kulishikia bango suala hilo kwa madai kuwa ‘Wakimataifa wamepanda daladala badala ya ndege’.

Lakini pamoja na hivyo kikosi cha Yanga kilichotua Shinyanga kipo kamili.

Wachezaji wa Yanga, waliosafiri na timu ni:


MAKIPA
Ally Mustafa ‘Barthez’, Benno Kakolanya na Deogratius Munishi ‘Dida’

MABEKI

Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Oscar Joshua, Kelvin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Andrew Vincent ‘Dante’ na Pato Ngonyani.




 


VIUNGO
Said Juma ‘Makapu’, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Simon Msuva, Obrey Chirwa, Yussuf Mhilu, Juma Mahadhi na washambuliaji Matheo Anthony, Malimi Busungu, Amissi Tambwe na Donald Ngoma.

Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh amesema mchezaji aliyebaki Dar ni Geofrey Mwashihuya ambaye ameanza mazoezi mepesi wiki hii kutokana na majeraha ya goti aliyopata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic