September 17, 2016

Straika Laudit Mavugo wa Simba amewatuliza mashabiki wa timu yake kwa kuwaambia leo atajitahidi na wenzake waifunge Azam FC halafu wageukie mechi nyingine zilizo mbele yao.

Simba ikiwa nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara inacheza na Azam ambayo ni ya kwanza kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku zote zikiwa na pointi 10 zikiwa pia zimelingana mabao ya kufunga na kufungwa.


  Akizungumza na Championi Jumamosi, Mavugo alisema: “Nipo fiti kwa ajili ya mchezo huu na jinsi tulivyo sasa, naamini tutashinda kwani hakuna haja ya kutoka sare mashabiki watulie wasiwe na wasiwasi.

“Tukishinda mechi hii tunatazama mechi zinazokuja ambazo pia tumepanga kushinda zote ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.”

Mavugo hadi sasa ana mabao matatu katika mechi nne za ligi kuu alizoichezea Simba akiwa amelingana kwa ufungaji na John Bocco wa Azam FC, Rafael Daud (Mbeya City) na Hood Mayanja wa African Lyon.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV