September 23, 2016


Mabingwa wa Kombe la Chalenji, Kilimanjaro Queens wamekuwa wakihaha kulipwa posho zao walizotakiwa kulipwa wakiwa nchini Uganda.

Queens wamekuwa wakihaha kulipwa posho zao bila ya mafanikio na imeelezwa wameonekana kukasirishwa.

Wachezaji wa timu hiyo ambayo ilibeba Kombe la Chalenji kwa Wanawake na kuwa ya kwanza kufanya hivyo kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, wamelalamika.

“Hatujapewa, wanatuzungumza na tulikwenda Airtel. Tumerudi pale TFF, bado wamekuwa wanatuhangaisha.

“Tunajisikia vibaya sana, tulipambana bila ya posho. Hasa mwishoni maana tulilipwa mwanzo tu kidogo. Sasa kwa nini watufanyie hivi,” alihoji mmoja wa wachezaji hao, huku akihofia kutojulikana.

“Ukweli tumeona kila wakati nahodha anakwenda pale kuuliza na kuambiwa baadaye. Mwanzo tulimkasirikia yeye, lakini mwisho tumeona hana makosa.”


Tw“Tumetoka Airtel kuja hapa, wamesema watatulipa leo. Lakini imeshindikana na vibaya zaidi wanatujibu vibaya, kweli hatujapenda.”


Imeelezwa, walilipwa posho za mwanzo tu, baada ya hapo walicheza mechi zote za mwishoni bila ya posho hadi walipofanikiwa kubeba ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic