September 23, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema hawawezi kukurupuka na kufanya maandalizi ya mechi dhidi ya Simba kabla ya kucheza na Stand.

Pluijm raia wa Uholanzi, amesema angependa wapambane kuhakikisha wanawashinda Stand kwanza.

“Baada ya hapo, yatafuatia mambo ya Simba. Hii ni ligi, unaanza na moja linafuatia jingine. Sasa tunajiandaa kucheza na Stand,” alisema Pluijm.


Yanga itaivaa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Jumapili. Baada ya hapo itafuatia mechi dhidi ya watani wake Simba, Oktoba Mosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV