September 20, 2016


Yanga itaweka kambi Pemba kujiandaa na mechi dhidi ya watani wake Simba, Oktoba Mosi.

Tayari mechi hiyo imekuwa gumzo nchini hata kabla ya timu hizo kumaliza mechi zao za wikiendi ijayo.

Taarifa zimeeleza, kambi ya Pemba imeonekana kuwa na baraka zaidi kwa Yanga ambayo msimu uliopita iliichapa Simba ‘nje ndani’.

“Kila kitu kinaonyesha hivyo, kambi itakuwa Pemba. Lakini ni suala la kusubiri sasa, tutajua nafikiri ndani ya siku mbili,” kilieleza chanzo.


“Hata kocha anavutiwa na kambi ya Pemba pia ushirikiano wa wanachama na mashabiki kule ni mkubwa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV