September 8, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameonekana kutofurahishwa na sare dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara, jana.

Yanga imekwenda sare ya bila kufungana dhidi ya Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara katika mchezo mzuri ambao ladha yake ilipunguzwa na uwanja mbovu.

Habari kutoka ndani ya Yanga, Pluijm amewaeleza wacheaji wake kuchukizwa na sare hiyo.

“Lakini ameonyesha kutuamini, amesema lazima tubadili mambo na kushinda katika mechi zijazo,” alisema mmoja wa wachezaji.
1 COMMENTS:

  1. Kwani ile Mipango inayowafanya washinde mechi zao bado haijaanza kutekelezwa?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV