September 17, 2016

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amethibitisha kuwa mastaa wake, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo wataukosa mchezo wa kesho Jumapili dhidi ya Espanyol katika La Liga.

Ronaldo ni mgonjwa wakati Bale anasumbuliwa na maumivu ya nyonga na hawakufanya mazoezi ya pamoja na wenzao kikosini hapo.


 "Cristiano hatasafiri na sisi amekuwa hajisikii vizuri, hatuna haja ya kufanya maamuzi magumu ya kumchezesha," alisema Zidane.

"Kuhusu Bale tunamuangalia, najua wachezaji wanahitaji kucheza lakini hatuwezi kufanya maamuzi hayo kwa kuwa bado michezo ni mingi, sina maana kuwa mchezo wa Jumapili siyo wa muhimu, hapana tunaweza kuwatumia kisha wakaumia zaidi," alisema.


 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV