September 17, 2016

Simba imeamua kukishtaki Chama cha Soka cha DR Congo (Fecofa) kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) baada ya kugomea kutoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya mchezaji wake, Mussa Ndusha aliyesajiliwa hivi karibuni.

Hadi sasa Ndusha pekee ndiye mchezaji wa kigeni wa Simba ambaye hajapata ITC kati ya waliosajiliwa katika dirisha lililofungwa hivi karibuni kufuatia Fecofa kukataa kutoa ITC yake.

Ndusha (kulia)
Awali Simba ilikuwa na mpango huo kutokana na Ndusha na Boukungu kutokuwa na hati hiyo, lakini licha ya hati moja kupatikana bado imeona msimamo uwe palepale kwenda mbele zaidi kutafuta haki yao.
 
Akizungumza na Championi Jumamosi, Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele alisema: 

“Wanachokifanya Fecofa ni utapeli wa kutaka kuitapeli Simba kwa kutaka wapewe fedha kwa mchezaji asiye na mkataba, tumelifikisha Fifa suala hili ili tupate haki yetu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV