Pamoja na kujifua gym, mshambuliaji nyota wa zamani wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu ameendelea kujifua mchangani.
Ulimwengu ameendelea na programu ya kufanya mazoezi mchangani, yote ikiwa ni kujiweka fiti baada ya kurejea nchini akiendelea kusubiri masuala yake ya kwenda kucheza soka barani Ulaya.
“Sasa programu ni mchangani, baada ya hapo nitaendelea zaidi,” alisema Ulimwengu.
Tayari amemalizana na TP Mazembe ambayo aliichezea kwa mafanikio makubwa na amenuia kwenda Ulaya na kupambana ili aweze kusonga zaidi.
Ulimwengu alitokea Ulaya katika klabu ya AFC ya Sweden kwenda kujiunga na TP Mazembe.
Maana yake akiende Ulaya atakuwa anarejea kwa kwa mara nyingine lakini safari hii itakuwa kwa kiwango cha juu.
0 COMMENTS:
Post a Comment