October 24, 2016

PLUIJM

Kocha Hans van der Pluijm ananukia Azam FC ambayo imeonyesha nia ya kumpa nafasi ya kuinoa.

Bado hakujawa na mwafaka kocha huyo raia wa Uholanzi, achukue nafasi ya kocha mkuu au mkurugenzi wa Ufundi.

Pluijm ametangaza kujiuzulu Yanga baada ya Kocha George Lwandamina kutua nchini na kumalizana na Yanga.

Lwandamina amemalizana na Yanga na anatarajia kuondoka na kurejea kwao Zambia kabla ya kurudi tena.

Lakini Azam FC imeonyesha nia ya kumnasa Pluijm ambaye iliwahi kumuwania hapo awali.

“Kuna mazungumzo ingawa inafanywa siri kubwa, sijajua sahihi ni mkurugenzi wa ufundi au kocha mkuu.

“Nafikiri ni suala ambalo linaendelea kushughulikiwa,” kilieleza chanzo.

Kumekuwa na ugumu kuwapata viongozi wa Azam FC lakini juhudi zinaendelea ili kupata kauli yao kuhusiana na Pluijm pia Kocha Zeben Hernandez raia wa Hispania ambaye anakinoa kikosi chao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV