October 10, 2016

PLUIJM

Yanga keshokutwa Jumatano itaikaribisha Mtibwa Sugar, lakini Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm ameingiwa na hofu na mbinu ya wapinzani wake kucheza soka la kibabe na nguvu nyingi ‘physical game’, hivyo ameshaanza kufanya maandalizi makini ya kukabiliana nao.

Mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi Kuu Bara, wapo nafasi ya sita na pointi zao 11, sita nyuma ya vinara wa ligi, Simba lakini Pluijm anasema ni mapema kuwatoa kwenye rada za ubingwa huo kwani kuna rundo la mechi ambazo zitaamua nani bingwa na si kwa sasa kwani nafasi ya kuutetea ipo.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Mtibwa, Mdachi huyo alisema ni moja ya timu zinazocheza soka la kibabe sana na nguvu nyingi, hali inayoweza kuwaathiri kwa kuumizwa kwa wachezaji wake, hivyo ameamua kulivalia njuga mapema ikiwemo mazoezi ya ufukweni juzi Jumamosi.

Pluijm alisema: “Mtibwa ni moja ya timu ngumu na nzuri, ni timu inayocheza soka la nguvu sana, mbinu inayokupasa kujipanga vema kuwakabili. Najua utakuwa mchezo mgumu lakini naamini tutapambana na kupata pointi tatu zitakazosaidia kutafuta taji letu.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic