October 12, 2016Baada ya kukanusha kwa muda mrefu kuhusu azimio la kocha wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ aliyetangaza kujiuzulu, hatimaye uongozi wa timu hiyo umethibitisha rasmi kuachana na kocha huyo.

Wiki mbili zilizopita, Julio alitangaza kujiweka kando kuifundisha Mwadui kwa kile alicholalamikia kuzidi kwa hujuma kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, hasa kwa upande wa waamuzi wa ligi hiyo.

Katibu Mkuu wa Mwadui, Ramadhani Kilao, aliweka wazi kwamba tayari wameshamalizana naye rasmi na kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya kocha msaidizi Khalid Adam, wakati ikielekea kwenye mchakato wa kumpata kocha mkuu mpya wa klabu hiyo.

“Rasmi nikwambie tu kwamba tayari tumeshamalizana kila kitu na Julio na kwamba, hatutaki tena kurudi nyuma zaidi sasa tunatazamia kumpata kocha mpya ambaye atapatikana Jumapili ya mwisho wa wiki hii mara baada ya kupitia baadhi ya majina ya makocha ambao tayari wameshatuma CV zao,” alisema Ramadhani Kilao.  


1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV