October 12, 2016

PLUIJM

Kama ilivyo kawaida yake Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru mwenye maneno mengi, ameibuka na kutamba kuwa wataifunga Yanga kupitia kwa beki wa kati wa timu hiyo, Andrew Vincent ‘Dante’ kwa kuwa wanamfahamu vilivyo na alikulia Mtibwa kabla ya kwenda Yanga.

Maneno hayo, yamemfikia Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm ambapo naye akasema atampanga beki huyo katika mechi hiyo na kumuongezea majukumu ya kuiangamiza Mtibwa kwa kuwa yeye anaifahamu zaidi na anajua hakuna fowadi wa Mtibwa anayeweza kumtingisha kijana huyo.

KIFARU
Pluijm, raia wa Uholanzi, amefunguka kuwa alichokisema Kifaru hakiwezi kuwa rahisi kwa kuwa Dante si beki wa mchezomchezo na ni mmoja wa mabeki bora kwa sasa, hivyo atampa nafasi kulithibitisha hilo mbele ya wengine pia wenye mashaka naye.

DANTE
“Hapana, nafikiri hiyo si sawa. Dante ni mmoja wa mabeki bora wa kati kwa sasa, anajiamini, ana ‘control’ nzuri, anajua kuusoma mchezo na anahimili dakika zote 90, sasa sidhani kama beki wa namna hiyo ni mwepesi kama anavyosema (Kifaru).


“Tutakutana uwanjani siku hiyo na najua Dante atacheza vizuri sana, kwanza anaifahamu Mtibwa na atakuwa chachu ya ushindi wetu, atakaba na atasaidia pia kuisambaratisha Mtibwa kwa namna ya mfumo wetu utakavyokuwa,” alisema Pluijm

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV