October 15, 2016


Takwimu za misimu mitatu zinaonyesha kuwa, safu ya ushambuliaji ya Yanga maarufu kama MTN imefunga mabao 102 na kuipiku ile ya Simba ijulikanayo kama Kiama.

MTN inaundwa na washambuliaji Simon Msuva, Amissi Tambwe na Donald Ngoma na ile ya Kiama inaundwa na Shiza Kichuya, Ibrahim Ajibu na Laudit Mavugo.

Ndani ya misimu mitatu, MTN imefunga mabao 102 wakati Kiama yenyewe ikiwa na mabao 99 na kuzidiwa mabao matatu tu na wapinzani wao.

KICHUYA

Ipo hivi, msimu wa 2014/15, Tambwe alikuwa amefunga mabao 14 nyuma ya kinara Msuva aliyefunga mabao 17 kabla ya msimu uliofuata kuibuka mfungaji bora akiwa na mabao 21.

Msimu huu tayari Tambwe ana mabao manne huku Msuva aliyefunga mabao tisa msimu wa 2015/2016 akiwa amefunga mabao mawili.

MAVUGO

Ngoma yeye katika msimu wake wa mwisho na FC Platinum ya kwao Zimbabwe kabla ya kutua Yanga, alikuwa amefunga mabao 16 na msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara alifunga mabao 17 na msimu huu ana mawili, jumla MTN ina mabao 102.

Kwa Kiama, msimu wa mwaka 2014/2015, Mavugo akiwa na Vital’O ya Burundi alifunga mabao 30, msimu uliopita alifunga 32 na sasa anayo matatu Simba. Ajibu yeye 2014/15 alifunga mabao nane, 2015/16 akafunga tisa na msimu huu anayo matatu.

Kinara wa ufungaji Kichuya yeye msimu wa 2014/15 hakuambulia kitu, ila 2015/16 alifunga nane na sasa ana mabao sita.


Jumla MTN ina mabao 102 na Kiama inayo 99, hivyo tofauti ya mabao matatu ndiyo iliyoiharibia Kiama kwa MTN.

2 COMMENTS:

  1. Umechemka, Mavugo, Ajib na Kichuya kwa pamoja wana magoli 13 tu kwenye ligi wakiwa pamoja. Hiyo hesabu yako ni very unrealistic. Unalinganisha vitu viwili tofauti. Tambwe, Msuva na Ngoma wana magoli yaiyofika kumi kwa mwaka huu, ambayo ndio ungeweza kuyatumia kulinganisha hizo safu mbili.

    ReplyDelete
  2. Umechemka, Mavugo, Ajib na Kichuya kwa pamoja wana magoli 13 tu kwenye ligi wakiwa pamoja. Hiyo hesabu yako ni very unrealistic. Unalinganisha vitu viwili tofauti. Tambwe, Msuva na Ngoma wana magoli yaiyofika kumi kwa mwaka huu, ambayo ndio ungeweza kuyatumia kulinganisha hizo safu mbili.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic