LIEWIG |
Uongozi wa klabu ya Stand United umeingia kwenye mgogoro mkubwa na kocha wake, Patrick Liewig ambaye ameamua kuondoka kikosini.
Liewig ameondoka katika kikosi cha Stand United kwa madai kwamba anadai mshahara wake wa miezi miwili na amekuwa akilipwa zaidi ya dola 5,000 (zaidi ya Sh milioni 11) kwa mwezi.
Imeelezwa baada wadhamini Acacia kujitoa kudhamini kutokana na mgogoro ulioanzishwa na wenye hamu ya kuipata Stand United, imekuwa kazi kubwa kumlipa kocha huyo.
Msemaji wa Stand United, Deo Makomba amethibitisha kuhusiana na Liewig kuondoka bila ya taarifa, lakini akasema wameshangazwa.
“Kocha anajua kila kitu, tulimueleza hali yetu kutokana na suala la wadhamini. Kwamba hatuko vizuri na baada ya miezi miwili tungemlipa.
“Lakini sasa ameondoka hotelini, tunamtafuta hatujui yuwapi! Tena kuna watu wanasema yuko Dar es Salaam, hili ni jambo linatushangaza sana.”
Kocha huyo ameifanya Stand United kuwa moto wa kuotea mbali msimu huu kwani baada ya mechi 9 ilizocheza, sasa iko katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment